Posts

KING KIBA AUAGA UKAPERA

Image
Nyota wa muziki wa Bongo flava nchini  Ali Saleh Kiba ameuacha rasmi ukapera baada ya kufunga ndoa na mpenziwe kutoka Kenya. Harusi hiyo ya kukata na shoka iliofanyika katika msikiti wa Ummul Kulthum ilihudhuriwa na rafiki wa mwanamuziki huyo Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho. Heart maker wa Seduce me aliisafirisha familia yake mjini Mombasa siku moja kabla ya kumuoa mchumba wake  Amina Ahmed 

JONAS MKUDE KUIKOSA LIPULI JONAS MKUDE AKIWA NA WACHEZAJI WENZIE

Image
Kikosi cha  wekundu wa Msimbazi ,Simba kushuka dimbani hii leo majira ya saa 10 kamili jioni  mjini Iringa kukipiga na Lipuli  FC   Uwanja wa Samora  Simba itakichakaza   bila kiungo wake Jonas Mkude ambaye anatumikia  adhabu ya kadi tatu za njano. Aidha Mkude atalazimika kusubiri mechi dhidi ya watani zake wa jadi utakaopigwa Aprili 29 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Pia Kiungo James Kotei ndiye atakuwa mbadala wa Mkude katika sehemu ya kiungo kutokana na kufanana aina ya mchezo wanaocheza.

NDALICHAKO KUITUMIA RIPOTI YA MDHIBITI WA HESABU KAMA CHACHU YA KUFANYA KAZI

Image
Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi, Joyce Ndalichako, amesema anaitumia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kama changamoto na chachu ya kuendelea kufanya kazi nzuri.  Ndalicho ameyasema hayo leo Aprili 17 wakati akijibu hoja za ripoti ya CAG iliyosomwa wiki iliyopita bungeni.  Wiki iliyopita mawaziri wanane walifanya mkutano na waandishi wa habari wakijibu hoja za ripoti ya CAG. “Serikali ya awamu ya tano kwenye suala la udhibiti haina utani kila mtu ameona kazi ambayo imefanyika, tunapopata ripoti ya CAG, inatupa chachu ya kuendeleza na kazi nzuri inayofanywa na serikali ya awamu ya tano,” amesema Amesema kama CAG alivyoshauri, watafanyia kazi mapendekezo ya CAG na pia watawachukulia hatua watendaji wanaotumia vibaya fedha za umma. Ndalichako alizungumzia hoja ya CAG kuhusu ukusanyaji hafifu wa fedha za mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu na akasema, tangu serikali ya awamo ya tano iingie madarakani, kumekuwa na ongezeko l...